Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini Tanzania (TFF) imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu inayojulikana kama Kagame Cup.
Baraza la Vyama vya Mpira
wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio wamiliki wa mashindano
haya na hutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki. Watatoa orodha ya
vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baade mwezi huu au mapema mwezi ujao.
Afisa habari wa TFF,
Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa wenyeji umetolewa na shirikisho
hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa.
Michuano hii inatarajiwa
kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
Michuano hiyo inadhaminiwa
na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi mwanachama
za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa
michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.