Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini
ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu
ya awali ya makundi.
Stars ambayo jana jioni
ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0,
imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa
na Swaziland, Madagascar na Lesotho.
Mara baada ya mchezo wa
jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema
amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya
kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij alisema, mpira wa
miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango
walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa hautazami
nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri
katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua
mazuri kwetu” alisema Nooij”
Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda
nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu,
na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo
kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu
kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el
Arab jijini Alexandria.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)