Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa (watatu kushoto mstari wa nyuma)
akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya mradi wa mawasiliano vijijini Awamu ya
2B ambapo makampuni ya simu ya TTCL, Vodacom na Tigo walisaini. Wanaosaini
kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Injinia Peter Ulanga, Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Rosalynn Mworia na Mwakilishi wa kampuni ya
MIC, Slyvia Balwire. Sherehe hiyo ilifanyika mkoani Dodoma jana.
Afisa Mkuu Mtendaji wa
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Injia Peter Ulanga akibadilishana hati za
makubaliano na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania
Rosalynn Mworia mara baada ya kusaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu
vijijini, katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) akiwa na Wawakilishi wa
makampuni ya simu yaliyosaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini
sherehe iliyofanyika mjini Dodoma jana. Wengine ni Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko
wa Mawasiliano, Aumsuri Moshi (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano Injinia Peter Ulanga. Mstari wa nyuma ni wawakilishi wa makampuni
hayo ya simu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura, Mwakilishi wa
Vodacom Tanzania, Rosaline Mworia na
Mwakilishi wa MIC Tanzania Ltd, Sylivia
Balwire.
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia,Prof Makame Mbarawa,(pili kushoto) akiwa na Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara
baada ya kampuni ya Vodacom kuwa kati ya makampuni matatu yaliyo saini mkataba
wa kupeleka huduma ya mawasiliano simu vijijini awamu ya 2B katika sherehe
zilizofanyika mjini Dodoma leo.