WINGA wa Simba, Ramadhani
Singano ‘Messi’, ameendelea kuwachunia viongozi wake licha ya kupewa mkataba
wenye thamani ya Sh milioni 30 badala ya milioni 50 ambazo winga huyo anataka
aweze kusaini.
Messi ameendelea kuzisikilizia timu za Azam na Yanga ambazo kila moja
imeonyesha kuhitaji huduma yake kutokana na kuwa katika kiwango kizuri kwa
misimu miwili mfululizo.Azam na Yanga kwa nyakati tofauti zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Itakumbukwa kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16, viongozi wa Yanga walionyesha nia yao ya kumuhitaji nyota huyo, lakini walisitisha mipango yao kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba na Simba.
Mbali ya Yanga kuonyesha nia ya kumtaka Messi, lakini pia uongozi wa Azam FC nao wameonekana kumwania winga huyo baada ya kufanya naye mazungumzo.
Simba imemtaka Messi
kutafakari juu ya dau la Sh milioni 30 badala ya 50 anazozitaka ambapo winga
huyo aliomba apewe muda zaidi kuweza kutafakari juu ya dau hilo kabla ya
kusaini.
Chanzo:Bingwaaa
Chanzo:Bingwaaa