Saturday, 9 May 2015

STEVE NYERERE KUWANIA UBUNGE


MWIGIZAJI na mchekeshaji katika tasnia ya filamu Bongo Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ anasema kuwa anatarajia kuingia katika kinyang’anyiro cha Ubunge huku lengo kuu kuwa sauti ya wasanii ambao anaamini wanakosa mtu wa kuwakilisha matatizo yao katika Serikali na anaona ni wakati muafaka yeye kuingia Bungeni.
“Naamini kabisa kuwa karibu na Serikali ndio mwanzo mwa kutatuliwa kwa matatizo yetu katika tasnia ya filamu na muziki pia, nitatangaza nia kuchukua moja kati majimbo makubwa kabisa hapa Dar, na kuingia Bungeni kwa kazi moja tu ya kutetea maslahi ya wasanii wote,”anatamba Steve Nyerere.


Msanii huyo anasema kuwa anasubiri muda wa kufunguliwa kwa kampeni na taratibu zingine ili aweke wazi kuwa ni Jimbo gani anagombea kupitia chama cha Mapinduzi kwani utaratibu hauruhusu kuanza kampeni mapema asije kupewa adhabu na kuharibu mchakato mzito aliopanga kuingia Bungeni