Sitti Abbas Mtemvu alishinda Taji la Miss TZ mwaka 2014, muda mfupi
baadae alitangaza kujivua Taji hilo baada ya mengi kusikika.. watu wakaandika
na kuhoji kuhusu umri wake, elimu yake, madai mengine ni yale kwamba ana mtoto…
aliwahi kuyajibu kwa nyakati tofauti, leo alikuwa Live kwenye show ya Nirvana
@EATV hii ni sehemu ya majibu yake.
“Niko sawa, nilikubaliana na changamoto nilizopitia.. namshukuru Mungu kwa kila kitu.. nina amani na furaha." Sitti Mtemvu.
Kilichomfanya akaamua
kuvua taji “Ilikuwa inaniathiri mimi na familia yangu… nikaamua nirudishe maana
maneno yalikuwa mengi“
Sitti anasema mdogo wake
aliumizwa pia na kila kilichomkuta yeye “Ilifikia hatua marafiki zake
shule wanamtania, walikuwa wanamwambia wewe ni mtoto wa ‘bibi bomba“
Kwani alilazimishwa kuvua
Taji? Uhusiano wake na Kamati ya Miss Tanzania ukoje? “Hapana, niliamua
acha nivue taji.. mimi na wao hatuna tatizo kabisa"
Iliwahi kuandikwa kwamba
ana uhusiano na Hasheem Lundenga, jibu lake je? “Hamna uhusiano wowote kati
yangu na Hasheem Lundenga, mengi yaliandikwa kama ilivyoandikwa mimi na mtoto,
it’s okay… yamepita”
Swali la umri je? “Nimeamua
kufunga huo ukurasa kwa sababu chochote nitakachokisema kitafunua mambo
yaliyopita.. nimeendelea mbele mimi sio Miss Tanzania nimeufunga huo ukurasa..
umri wangu ni kitu binafsi”