Fela ametoa maneno hayo
kupitia ukurasa wake wa Facebook wakati akimpongeza Dogo Aslay katika
siku yake ya kuzaliwa. Mkubwa Fela akampa usia mzito Dogo Aslay pamoja na
kumshukuru na kumpongeza kwa juhudi za ushirikiano wake uliosaidia kuisimamisha
vilivyo Mkubwa na Wanawe pamoja na Yamoto Band.
Katika maandishi yake
hayo, Fela akafichua kuwa ujenzi wa nyumba za waimbaji wote wanne wanaounda
Yamoto Band uko ukingoni na panapo majaaliwa watakabidhiwa mwezi Julai mwaka
huu.
Mtaandao huu unakuwekea
maneno yote ya Said Fela neno kwa neno bila kuongeza wala kupunguza
kitu na baada ya hapo kiroho safi kabisa tumpe pongezi zake.
Happy birthday mwanangu Aslay Isihaka mwanangu sina cha kukuusia ila MUNGU alishakupa Imani na upendo ila natakiwa nikuongoze na mafanikio yako wadau wayaone nikitamka ivi kama ada yangu kwenye moyo wangu. Nilikushauri kusapot wenzio hukubisha mpaka tumetengeneza Yamoto Band mpaka leo umefunga pini mpaka umewatobolesha wenzako Beka, Maromboso na Enock Bella pia kukitambulisha kituo chetu cha Mkubwa na Wanawe nchini na kwenginepo duniani. Najua kuna wadau wanapenda kujua mpaka sasa umefaidika nini wewe napenda kuwafamisha japo upendagi, ulisomeshwa na Mkubwa Fela na ulipata nyumba ya kwanza 2013. Na tangu tuiazishe Yamoto Band ulitoa wazo ulisema mkubwa kama unavyojua familia tulipotokea naomba tutengenezee kota zetu zifanane ata tukizeeka tuwakumbuke. Asante wazo lako tumelifanyia kazi ujenzi unafikia mwisho na INSHAALLAH tunafanya mipango mimi na viongozi wenzangu wa Mkubwa na Wanawe Youth Centre tumpate mh raisi wetu wa jamhuri ya Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE mwezi wa 7 awakabidhi nyote Yamoto Band nyumba zenu, muhimu tuombe dua INSHAALLAH happy birthday Aslay.