MREMBO mwenye sauti
nyororo kutoka Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Winifrida Josephat ‘Recho
Mapenzi,’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio baada ya kuzuiwa kupanda
kwenye jukwaa kwa ajili ya kumtunza Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz.’
Mrembo mwenye
sauti nyororo kutoka Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Winifrida Josephat
‘Recho Mapenzi.
Tukio hilo
lilitokea ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kwenye shoo ya Zari All
White Party ambapo bidada huyo akiwa katika hali ya mzuka alijikuta akiishia
kuangua kilio baada ya kuzuiwa na Meneja wa Diamond, Babu Tale kupanda
jukwaani.
Akilalama kwa
machungu baada ya kukwamishwa kumfikia Diamond, Recho alisema kuwa
hakufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Babu Tale kwani anamjua wazi ni msanii
hivyo hakuwa na haja ya kuwaamuru mabaunsa kumzuia kwenda kumtuza staa
mwenzake.
“Kweli Tale
hajanitendea haki hata kidogo, kwani nilimuahidi mapema Diamond ningemtuza na
pale nilitaka kutimiza ahadi yangu lakini nikazuiwa,” alisema Recho kwa
masikitiko