Msanii mrembo na mwenye
mvuto katika tasnia ya filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’
amefunguka kuwa anapenda kuwa na mahusiano na wanaume wanaomzidi umri kwa
sababu wanakuwa na nafasi nyingi katika maisha yake.
Akihojiwa amesema kuwa
anapenda kuwa na wanaume wanaomzidi kwa sababu wana nafasi tatu katika maisha
yake ya kawaida, hazo ni kuwa kama kaka, baba na mpenzi.
Ameongeza kuwa hawezi kuwa
na mwanaume ambaye wanalingana umri kwa sababu atakuwa hana sifa hizo pia akili
zao zitakuwa hazijakomaa na hivyo kushindwa kushauriana katika kufanya vitu
vingi vya maendeleo.