Tuesday, 12 May 2015

KINONDONI TALENT SEARCH YAANZA KWA KISHINDO


Hiki ni kitu kikubwa ambacho kimeletwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni, DC Paul Makonda ambapo kila mwenye kipaji ana nafasi ya kushiriki mashindano haya ili kuonesha uwezo wake kwenye kuigiza, kuimba, kuchekesha na kucheza nafasi ndio hii.

Mashindano yameanza rasmi leo pale Coco Beach, tayari washiriki wameanza kuonesha vipaji vyao na mashindano hayo yataendelea kwa siku tatu.