Saturday, 9 May 2015

KAJALA: SITOSAHAU MSAADA WA WEMA SEPETU KAMWE

Kajala Masanja amesema kuwa pamoja na kuwa hawana waelewano mazuri na rafiki yake wa zamani Wema Sepetu, hawezi kusahau wema aliomfanyia wa kumtolea shilingi milioni 13 kwenye huku yake miaka kadhaa iliyopita.
Kajala amesema hafikirii kuzirudisha fedha hizo kwa Wema ambaye amekuwa akieleza kujuta kuutoa msaada huo.

“Sio kwamba natamani kumrudishia milioni 13, kwa sababu mimi najua yeye alinisaidia kipindi mimi naHitaji na hakuna mtu yoyote alitokea kunisaidia kipindi hicho,” Kajala aliiambia Global Online TV .


“Kweli nashukuru mpaka kesho kwa sababu alitoa msaada ambao siwezi kuusahau hata kama tuna ugomvi kiasi gani. Sasa kwa sababu yeye alisaidia kwa moyo mmoja na akikaa akiongea anajuta kwanini alinisaidia kumlipia Kajala inakuwa inamfutia hata zile baraka alizozipata.”


Pia Kajala pia alieleza kuwa yeye na Wema wanaweza kurudi kuwa pamoja kama zamani ila sio kwa kufuata ushauri wa watu mitandaoni bali ikitokea kila mmoja amemiss mwenzake wataongea na yataisha.