Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) imeshusha nauli za
mabasi ya masafa marefu huku nauli za daladala viwango vyake
vikibaki kama kawaida.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushushwaji wa nauli za mabasi ya masafa marefu ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA),Gilliard Ngewe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jijini Dar es salaam leo.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Udhibiti usafiri wa barabara,Geffrey Silinda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe.
Ngewe
amesema uamuzi huo umekuja baada ya mamlaka hiyo kufanya utaratibu wa kupitia
kanuni kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo watoa huduma ili kutoa maoni
yao,kutokana na ongezeko la msongamano wa magari mijini.
Viwango
vilivyobainishwa kutokana na ukokotoaji wa nauli mpya za mabasi ya mijini ni
pamoja na;
0-10km nauli ya sasa ni Sh.400 sawa na asilimia 5.811-15km nauli ya sasa ni Sh.450 sawa na asilimia 0.316-20km nauli ya sasa ni Sh.500 sawa na asilimia 2.921-25km nauli ya sasa ni Sh.600 sawa na asilimia 2.826-30km nauli ya sasa ni Sh.750 sawa na asilimia 1Huku nauli ya Mwanafunzi ikibaki palepale sh.200
0-10km nauli ya sasa ni Sh.400 sawa na asilimia 5.811-15km nauli ya sasa ni Sh.450 sawa na asilimia 0.316-20km nauli ya sasa ni Sh.500 sawa na asilimia 2.921-25km nauli ya sasa ni Sh.600 sawa na asilimia 2.826-30km nauli ya sasa ni Sh.750 sawa na asilimia 1Huku nauli ya Mwanafunzi ikibaki palepale sh.200
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo)
Wakati
viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu ni pamoja
na;Daraja la kawaida la chini kwa Barabara za Lami ,viwango vipya
vilivyoridhiwa ni 34.00 TZS/Abiria/km sawa na 7.8%Daraja la kawaida la chini
kwa Barabara za vumbi ,viwango vipya vilivyoridhiwa ni 42.50 TZS/Abiria/km sawa
na 7.8%Daraja la kawaida la juu, kiwango kilichoridhiwa ni 44.96TZS/Abiria/kmDaraja
la kati,viwango vilivyoridhiwa ni 50.13TZS/Abiria/km sawa na 5.81%Aidha,Bodi
hiyo ya Wakurugenzi imeamua kwamba nauli za mabasi ya hadhi ya juu (Luxury bus)
hazitadhibitiwa ili kuchochea ubunifu katika utoaji huduma na ushindani kati ya
huduma za barabara na njia njinginezo za usafiri.