Thursday, 16 April 2015

NASH MC: TUSIDANGANYWE TUKAPOTEZA AMANI YETU


Msanii wa Hip Hop Bongo anayefanya poa sana kwa ngoma zake kibao kama ‘Zima’, Nash MC aka Mchochezi ameamua kufunguka vikali kupitia ukurasa wake wa Facebook juu ya matukio yanayotokea hapa Tz.

“Kaka na dada zangu watanzania nawaomba tuwe makini sana, kuna mipango inafanywa ya kutogombanisha watanzania kupitia dini hasa waislamu na wakristo kuna baadhi ya matukio ni wazi kabisa yanapangwa na watu au mataifa ya nje kwa maslahi yao binafsi, tumeishi miaka mingi pamoja bila ya matatizo ya aina yoyote kwa muda mrefu, tunashirikina kwa mambo mengi  tu lakini inaonekana wazi wapo baadhi ya watu au mataifa yanayopanga haya mambo, mfano tumeona kwa wenzetu wa nchi ya Afrika ya kati jinsi walivyoingia kwenye vita vya kidini na kusababisha maafa na vifo vya maelfu ya watu”

Mwenyezi Mungu tunusuru.