Baada ya Zitto kutoa kauli kwa vyombo vya habari kuwa, kuna zaidi ya
wabunge 50 kutoka vyama vya CCM na CHADEMA watakao hamia ACT, CHADEMA kupitia
kitengo chake cha intelijensia kimetangaza upelelezi rasmi ili kuweza
kuwavumbua wabunge hao wasaliti wa chama na mamluki wengine!
Aidha, maofisa hao katika kitengo hicho cha intelijensia cha CHADEMA
wameeleza wazi kuwa wanaifanya kazi hiyo kwa usahihi na umakini mkubwa ili
kuhakikisha taarifa watakazokusanya ni za kweli huku wakielezea mkakati wao wa
kupenyeza watu wao ndani ya ACT kwa ajili ya taarifa zaidi!
My take,
Kwa hali hii, nadhani CHADEMA imeanza kusahau jukumu lake la msingi la
kufanya siasa na kujenga chama, badala yake nguvu nyingi zaidi imeelekezwa
kwenye kusaka hao wanaoitwa 'wasaliti'!
Mbona CCM ina watu wanatofautiana kimtazamo lakini maisha ya siasa yanaenda
kama kawaida na hatusikii majina majina kama wasaliti?