Mgomo wa Madereva umeanza rasmi leo
katika maeneo mbalimbali nchini kama ambavyo
muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero
zao na serikali.
Sababu kubwa ya madereva hao kugoma
ni kuishinikiza serikali kuweka mfumo mzuri
wa ajira na kupinga kanuni inayowataka
kurudia kusoma katika chuo cha taifa
cha usafirishaji,NIT kila leseni zao
zinapokwisha muda.
Madereva hao wanadai malalamiko yao
makubwa ni kitendo cha Serikali kuongeza
kifungu kidogo katika sheria mpya ya
mwaka 2015 namba 31 inayowataka madereva
wote wenye leseni za madaraja E,C1,C2,C3
na C kurudi darasani kila baada ya
miaka mitatu kuongeza utaalamu katika fani
hiyo ya udereva ili kupunguza ajali
za mara kwa mara zinazotokea
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungu huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana
kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna
uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj
zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo
asubuhi.