Friday, 17 April 2015

Kwa Kauli Hii, Uwoja Ana Ujauzito?


Staa mrembo wa Bongo, Irene Uwoya amewaacha njia panda mashabiki wake baada ya kubandika picha mtandaoni akionekana yupo bafuni  akiwa amejishika tumbo na kuiandikia maneno akiwatata mashabiki wamtajiae majina mazuri ya kike.

“Ntajie majina mazuri yakike unayoyapenda.....”- Uwoya aliandika.

Kauli hii ilizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wakioji kama mrembo ambae ni mama wa mtoto mmoja kama anaujamzito au la, wengine walienda mbali zaidi wakisema kuwa inawezekana akawa ni mjauzito na anatarajia kujifungua mtoto wa kike.

Mbali komenti nyingi kumtaka atoe maelezo zaidi juu ya hili, Uwoya hakujitokeza kusema lolote hivyo hadi sasa mashabiki wake wapo njia panda wakijiuliza, …ana ujauzito au hana?

Swaga kama hizi ya mtandaoni huwa mara nyingi zina maaanisha picha picha za tumbo zimekuwa nyingi sana kutoka kwa mrembo huyo. ngoja tuendelee kusubiri kwani hili ni jambo la kheri. 
Ad