Tuesday, 28 April 2015

HAYAWI HAYAWI SASA YATATIMIA..!! NDOA YA WEMA SEPETU YAWA GUMZO LA JIJI


Ubuyu Mpya unaoenea kwa siri kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa, ni kuhusu ndoa ya super star wema sepetu inayotarajiwa kufungwa ivi karibuni. Chanzo cha ubuyu kinaeleza kuwa hatua zote muhimu zimeshachukuliwa, kinachosubiriwa tu ni bwaba harusi huyo mtarajiwa kuchukua jiko lake bila kipingamizi chochote. Mpaka sasa ivi bado mume huyo mtarajiwa wa staa huyo hajawekwa wazi kwa kuogopa watu wabaya kumfanyia fitna.

Mpaka sasa management yake inafanya siri kubwa kuhusu tukio hilo muhimu litakalobadilisha title na heshima ya msanii huyo.