Hatimaye chama cha
CHADENA kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake Zitto Kabwe.Mahakama
Kuu (Mziray,Judge) amekubaliana na hoja za wanasheria wa CHADEMA za
pingamizi dhidi ya case hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa
kisheria. Mahakama Kuu imeipa CHADEMA gharama zote za kuendesha case hiyo. Kwa
maana hiyo hakuna shauri lolote Mahakamani kwa sasa kuhusu suala hilo.
Aidha, Mahakama imeamuru Zitto alipe
gharama zote za kesi.
Wanasheria wa chama, Peter Kibatala
na John Mallya na Tundu Lisu wanatarajiwa kuongea na Vyombo vya Habari
hii leo.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka
pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili.
Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati
kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize
kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa
yake