“Wakati
wa sakata la Escrow bungeni, kuna mjumbe mmoja wa PAC aliitwa na vinara wa
watuhumiwa wa Escrow na kutakiwa kusema uongo bungeni kuhusu mimi kwa ahadi ya
kupewa donge nono, mjumbe huyo alikataa, na hapo ndipo vinara hao wa Escrow
wakaapa kutenga Shilingi Milion 500 kwa kila jimbo la kila mjumbe wa PAC
kuhakikisha kuwa wajumbe hao wote hawarudi bungeni.
Kwahiyo nahisi kuwa hiki kilichonitokea sasa ni sehemu ya mkakati huo maana sakata la escrow limegusa wengi, hadi majaji wamo.”
“Kama Katiba ingebadilishwa kabla ya uchaguzi mkuu 2015 na ikaruhusu mgombea urais mwenye umri chini ya miaka 40, ningegombea urais, nahitaji kuongoza nchi, kwa ubunge imetosha, lakini kwa kuwa haiwezekani, nitagombea ubunge lakini si Kigoma Kaskazini, nitatafuta jimbo linguine la kugombea ili nao nikawatumikie, Kigoma Kaskazini nimeshafanya kila kitu, sitakuwa na jipya”
Hajasema atagombea kupitia chama gani,