Tuesday, 10 March 2015
Flora Mbasha Atoa Ushahidi wake Kwa Siri Kuhusu Kesi ya Ubakaji Inayomkabili Mumewe, Emmanuel Mbasha
Kesi ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.
Kesi hiyo ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale
ya saa 5 hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.
Siku hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana.
Mbasha anashtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara nyingine eneo hilohilo.