Wiki iliyopita kulikuwa na vichwa vya habari kuhusu Baraza la Sanaa Taifa kutoa barua ya Onyo kwa msanii Shilole baada ya kuonekana akiwa wazi sehemu za juu ya mwili wake jukwaani kwa bahati mbaya kwenye show yake aliyoenda kuifanya Ubelgiji.
Shilole na Snura ni
watu ambao wanafananishwa na kupambanishwa na wakati mwingine kulinganishwa
kwenye muziki wanaoufanya.. millardayo.com imepata nafasi ya kuongea
na Snura kuhusu hili lililomtokea Shilole.
Snura ameanza
hivi>>’Kiukweli kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi kutoka
kwenye moyo wangu namuombea sana msamaha na Watanzania wasimuangalie hivyo
ambavyo wanamuangalia‘
Sentensi nyingine Snura amesema>>’Ile
ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu mzima
na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza ni kama
unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona je itatokea tena?‘