Wednesday, 11 March 2015

Bob Junior: Sikupenda Ndoa Yangu Ivunjike


Msanii na mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records, Bob Junior amesema hayakuwa mapenzi yake kuacha ndoa yake ivunjike.

Bob Junior ameiambia Bongo5 kuwa kilichotokea ni majaliwa ya mwenyezi Mungu.
“Nitaoa lakini sio miaka ya karibuni ni miaka ya mbele sana kwa sababu niliingia kwenye ndoa halafu mwisho wa siku ndo haikukaa muda mwingi ikanishinda,” amesema.

 

“Yaani siwezi tena kusema niache halafu nione tena, simaanishi kwamba ndoa ya kwanza nilikurupuka, ilitokea kwa neema za Mungu na bahati mbaya kwa majaliwa ya Mungu ikavunjika. Watu wanauliza sana hili suala lakini mimi nipo single kabisa. Mimi nashangaa watu wanaendelea kuniuliza,” ameongeza.