Wednesday, 11 March 2015

Lady Jaydee - Sina mimba, Mniache.




Lady jaydee amekasirika ni baada ya followers wake kumhisia kuwa ana ujauzito kutokana na picha aliyoweka instagram. Kupitia ukarasa wake wa instagram, Lady Jaydee ameandika:

“Imebidi nifute post, ili nielezee upya, hivi watu hamuelewi Kiswahili au ni nini???? Nmesema tumbo limevimba sababu ya sahani, nikimaanisha mlo na nilipost nakula hapo awali, sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi?, Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Raisi atakaewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba, Hebu niacheni basi khaaa, Nisiishi kisa mimba? Aisee mnaboa sana, Basi niueni kisa sijazaa, ili niwaondelee kero kabisa"