Friday, 13 March 2015

Alichosema Kamanda Kova kuhusu tukio la kutaka kuawa kwa sumu Dr. Slaa


Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na uchunguzi dhidi ya Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk.Wilbrod Slaa anayedaiwa kufanya njama ya kumuua kwa sumu, Bw. Khalid Kagezi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema wamechukua maelezo kwa Katibu Mkuu Dk.Wilbrod Slaa pamoja na maelezo ya mlizi wake Khalid Kagezi.
Kamishina Kova amesema Chadema walichukua hatua mbalimbali na kujiridhisha kuhusika kwa mlinzi wa Dk.Slaa kufanya mikakati ya kumuua kwa sumu kwa kuiweka katika maji au chakula.

Amesema kwa maelezo ya Mlinzi huyo alidai kuteswa na baadhi ya watu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwataja kwa majina.

Kamishina Kova amesema Kagezi alidai kutekwa na kushambuliwa katika mwili wake na jeshi la Polisi likampa fomu namba tatu (PF3)kwa ajili ya matibabu
“Jeshi la Polisi limefanya jitihada kwa kupata maelezo kwa watu wote ambao wamehusika kwa mlizi na Dk.Slaa”amesema Kamishina Kova.
Amesema baada ya uchunguzi watapeleka kwa wakili wa serikali