MODO maarufu Bongo, Agness Gerad ‘Masogange’ ameshtushwa na ushindi wa makalio yake baada ya kutojua kama ametajwa kuwa ni mwanamke mwenye makalio mazuri Afrika Mashariki.
Masogange alishinda nafasi hiyo kupitia utafiti
uliofanywa na mtandao wa Media Take Out ambapo kwa kutumia vigezo vyao,
walimwanika Masogange kuwa ndiye mwanamke pekee mwenye makalio bomba wakidai
amejengeka vizuri zaidi.
“Daah! Mimi mwenyewe nilikuwa sijui, nashukuru kama wao wameona mimi ndiyo mwenye kiungo hicho muhimu cha kuvutia na bora kwa wanawake wengine wote,” alisema Masogange ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake nchini Afrika Kusini.