Baada ya kukosa michuano ya ulaya kwa msimu uliopita,
hatimaye usiku wa leo Manchester United imerejea rasmi katika michuano hii
mikubwa barani humo kwa ngazi ya vilabu.
Vijana wa Louis Van Gaal walisafiri mpaka Uholanzi, nyumbani
kwa kocha wao, kucheza na klabu ya PSV.
Mchezo huo umemalizika kwa Manchester kupata mapigo mawili
kutoka kwenye mechi hiyo, baada ya kukubali kipigo cha 2-1 na pigo lingine
ikiwa ni kuumia vibaya kwa mchezaji wao tegemeo Luke Shaw.
Manchester United walianza kuliona lango la PSV katika
dakika ya 41, goli likifungwa na kijana aliyenunuliwa kutoka PSV – Memphis
Depay, lakini sekunde kadhaa kabla ya mchezo kwenda mapumziko PSV wakasawazisha
kupitia kwa Moreno.
Kipindi cha Narsingh aliifungia PSV goli la ushindi katika
dakika ya 57.
MATOKEO YA MECHI NYENGINE