Saturday, 20 June 2015

JACOB STEVEN (JB) AKANUSHA KAULI ZA KUGOMBEA UBUNGE K'NDONI



 
Msanii wa filamu nchini Jacob Steven amekunusha kauli ya kutaka kugombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni, kauli hiyo ameitoa mara baada ya kuzuka maneno hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kuwa ana nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu 2015. 
Akijibu suali hilo aliloulizwa na shabiki wake@mrekebishatabia Kupitia akaunti yake ya instahgram Jb amesema..

“NA MIMI NIMEZISIKIA HABARI IZO ETI NATAKA KUGOMBEA KINONDANI. SI ZA KWELI INGAWA KUNA KUNDI KUBWWA LILINIFATA NA KUNISHAWISHI NIGOMBEE LAKINI NILIWAJIBU NASHUKURU KWA KUNIFIKIRIA LAKINI NAFURAHIA KAZI YA UIGIZAJI KULIKO KAZI NYENGINE”