Sunday, 24 May 2015

WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI MKOANI MBEYA LEO


Watu watatu wamepoteza maisha leo baada ya basi la abiria liitwalo Super Feo linalofanya safari zake toka Mbeya Songea baaya ya kupata ajali maeneo ya Inyara mkoani Mbeya likiwa na abiria 20. 

Habari zinasema dereva wa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 53 kutaka kulipita gari lingine bila ya uangalifu ambapo akakutana na roli mbele yake hivyo katika kujiokoa akakimblia kulia zaidi ndipo basi likapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvati.

Waliotajwa kupoteza maisha ni Anastazia Ngonyani, Robert Lyman kutoka Marekani na mwanaume ambaye bado hajafahamika jina.

Abiria 13 wako salama dereva wa basi anaitwa shafii ngaiyo ametoroka baada ya tukio.

Taarifa zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na Patriki Mwimbila dereva msaidizi wa basi hilo ambaye amevunjika mguu.

Majeruhi wengine waliotajwa na ambao wote wamelazwa katika hospitali ya ru faa ya Mbeya ni Sakeni mwandanege, Fatuma nyambi na Feliciana mwalongo.