Friday, 29 May 2015

WASHINDI WA BSS WANALIPWA PESA TASILIMU

Chief judge na mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark production inayoandaa shindano la muziki la Bongo star search “Ritha Paulsen” amesema uvumi unaoenea mitaani kwamba huwa hawalipi pesa washindi wa shindano hilo ni wakupuuzwa. 
Akifunguka jijini Dar es Salaam Madame amesema taarifa hizo zinalengo la kuwachafua na kwamba kama kweli wangekuwa hawalipi basi BASATA ingewafungia.

“Shindano la bongo star search ni mwaka wa nane tunafanya, nafikiri tungekuwa tushafungiwa kawaida zawadi hizo tunaziwakilisha kwa BASATA, waulizwe hata hao wanaochukua watakwambia si kweli” alisema Ritha.

Katika line nyingine Madame amefunguka kuwa, shindano hilo litafanyika kama kawaida mwaka huu na kipindi kipya ambacho kitaitwa Ritha Paulsen show.