Polisi nchini Marekani
wamesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye
silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika mkahawa mmoja katika mji wa Waco.
Hata hivyo watu wengine 18 walipelekwa hospitali
kupatiwa matibabu kutokana shambulio hilo. Maofisa katika mji huo wanasema kuwa
walibaini mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la
kawaida. Watu waliokuwa katika mkahawa huo walijificha katika chumba cha
majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka katika
eneo hilo.