Tuesday, 19 May 2015

OBAMA AJIUNGA NA TWITTER, IKULU YA MAREKANI YATHIBITISHA.


Rais wa Marekani Barack Obama amejiunga na mtandao wa twitter, ikulu ya White House imethibitisha.

Akitumia anuani @POTUS (President Of The United States) Obama tayari amewavutia wafuasi 1.7 milioni moja nukta saba.

"Hamjambo, Twitter!Ni Barack.

Kwa hakika baada ya miaka 6 hatimaye wameniruhusu kujiunga na mtandao wa Twitter''Obama alisema kwenye ujumbe wake wa kwanza.

Obama alikuwa na anuani tofauti inayomilikiwa na wahudumu wa ikulu yake .Anuani hiyo inawafuasi Milioni 59.3m.

Anuani hiyo @BarackObama ilizinduliwa mwaka wa 2007, na kila akituma ujumbe anaanza na BO.

" Anuani ya @POTUS itamruhusu Obama kuwasiliana moja kwa moja na mamilioni ya wafuasi wake'' ilisema taarifa ya White House .

"Rais Obama angependa serikali yake iwe ya wazi @POTUS na hii ndio jukwaa mwafaka ya mazungumzo."

Kwa sasa rais Obama amewafuata watu 65 wakiwemo rais wa zamani wa Marekani ,Bill Clinton, George Bush na mkewe mwenye anuani ya kipekee @FLOTUS.

Hata hivyo hajamfuata Hillary Clinton wala waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.

Tayari mawasiliano yake na Bill Clinton yamezua mjadala Clinton akimtania kwa kumuuliza iwapo ataondoka na anuani hiyo atakapo achia ngazi naye akam