Saturday, 16 May 2015

MOE MUSIC NAYE ALIA JUU YA TUZO ZA KILIMANJARO

BAADA ya icon wa muziki wa Bongo Flava kwa sasa Naseeb “Diamond” Abdul, kuandika waraka mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram pamoja na Facebook kuhusu kusikitishwa kwake na baadhi ya wasanii kuachwa katika vipengele vya tuzo za muziki za Kilimanjaro mwaka huu, kwa kile anachokiamini kuwa wamefanya vizuri kwa mwaka 2014.
Miongoni mwa wasanii aliowataja Diamond ni mwanamuziki zao la mkoa wa Mwanza Moe music, ambaye amefanya vizuri sana mwaka jana kama msanii chipukizi lakini matokeo yake hakuwekwa kwenye kipengele anachostahili cha msanii chipukizi.

Mwandishi wa story hii aliweza kuzungumza na  Moe Music ili kufahamu jinsi alivyoupokea waraka huo, lakini pia mtazamo wake kuhusu tuzo za Kilimanjaro mwaka huu. Mkali huyo wa Hit single ya “basi nenda” amefunguka kuwa, ameumizwa na ameshangazwa sana na kilichotokea kwa sababu yeye alistahili kuwepo kwenye kwenye msanii bora chipukizi na wimbo bora wa mwaka “basi nenda”.

“Kwanza mimi sikuiona ile, kuna mtu tu ali screenshot na baadae nikaona Ney wa Mitego, Wolper, Kipindi cha Mseto Kenya wamerepost ile post ya Diamond

Unajua mimi sikutaka kuongea ,nilitaka mashabiki na watu waseme iliyokweli kwa sababu waandaaji wa tuzo wame cheat(wamedanganya) wazi wazi na watu wameona, na watanzania sasa hivi wameamka wanajua

Na nikaona tu picha eti nimetuma muwakilishi hapana si kweli sikumtuma mtu yeyote Yule ila nawashukuru BASATA na Kilimanjaro kwa hili na mashabiki kwa kufunguka ukweli wa mambo” alisema Moe Music.

Katika line nyingine Moe ameshangazwa na BASATA kuuweka wimbo wa “basi nenda” kama wimbo unaoshindania wimbo bora wa Zouk rhumba, kwa kuwa wimbo wake hauna mahadhi hayo na watanzania hawajui huu mziki wa Zouk Rhumba.

“Yaani ati nimeshangazwa tena unajua bro mtaani hawajui hii zouk sijui, na mziki wangu si huu hata hiki kipengele pia wamecheat hapa, tuliandika barua yakutokushiriki lakini hawakutuzingatia” alimaliza MoeBAADA ya icon wa muziki wa Bongo Flava kwa sasa Naseeb “Diamond” Abdul, kuandika waraka mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram pamoja na Facebook kuhusu kusikitishwa kwake na baadhi ya wasanii kuachwa katika vipengele vya tuzo za muziki za Kilimanjaro mwaka huu, kwa kile anachokiamini kuwa wamefanya vizuri kwa mwaka 2014.

Miongoni mwa wasanii aliowataja Diamond ni mwanamuziki zao la mkoa wa Mwanza Moe music, ambaye amefanya vizuri sana mwaka jana kama msanii chipukizi lakini matokeo yake hakuwekwa kwenye kipengele anachostahili cha msanii chipukizi.

Mwandishi wa story hii aliweza kuzungumza na  Moe Music ili kufahamu jinsi alivyoupokea waraka huo, lakini pia mtazamo wake kuhusu tuzo za Kilimanjaro mwaka huu. Mkali huyo wa Hit single ya “basi nenda” amefunguka kuwa, ameumizwa na ameshangazwa sana na kilichotokea kwa sababu yeye alistahili kuwepo kwenye kwenye msanii bora chipukizi na wimbo bora wa mwaka “basi nenda”.

“Kwanza mimi sikuiona ile, kuna mtu tu ali screenshot na baadae nikaona Ney wa Mitego, Wolper, Kipindi cha Mseto Kenya wamerepost ile post ya Diamond

Unajua mimi sikutaka kuongea ,nilitaka mashabiki na watu waseme iliyokweli kwa sababu waandaaji wa tuzo wame cheat(wamedanganya) wazi wazi na watu wameona, na watanzania sasa hivi wameamka wanajua

Na nikaona tu picha eti nimetuma muwakilishi hapana si kweli sikumtuma mtu yeyote Yule ila nawashukuru BASATA na Kilimanjaro kwa hili na mashabiki kwa kufunguka ukweli wa mambo” alisema Moe Music.

Katika line nyingine Moe ameshangazwa na BASATA kuuweka wimbo wa “basi nenda” kama wimbo unaoshindania wimbo bora wa Zouk rhumba, kwa kuwa wimbo wake hauna mahadhi hayo na watanzania hawajui huu mziki wa Zouk Rhumba.

“Yaani ati nimeshangazwa tena unajua bro mtaani hawajui hii zouk sijui, na mziki wangu si huu hata hiki kipengele pia wamecheat hapa, tuliandika barua yakutokushiriki lakini hawakutuzingatia” alimaliza Moe