Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amesema dhana ya uwazi
katika kuwahudumia wananchi isiwe kwa taasisi za serikali peke yake, bali pia
hata kwa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Rais wa Tanzania Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete, amesema dhana ya uwazi katika kuwahudumia wananchi isiwe
kwa taasisi za serikali peke yake, bali pia hata kwa asasi za kiraia na
mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo kwa pamoja yana jukumu la kuwahudumia
Watanzania.
Akizungumza katika mkutano
wa kimataifa wa ubia katika uwazi serikalini, Rais Kikwete amesema inashangaza
kuona jamii inakuwa na mtazamo potofu pale serikali inapozitaka asasi za kiraia
kuweka wazi utendaji wake, kwani amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa mashaka
waliyonayo wananchi juu ya utendaji wa asasi hizo.
Rais ametolea mfano wa
matumizi mabovu ya rasilimali zinazokwenda kwa asasi za kiraia na kwamba dhana
ya uwazi ni muhimu hasa kipindi hiki ambapo kiasi kikubwa cha misaada na pesa
za wahisani zinazoletwa nchini zinapitia kwa asasi za kiraia.
Aidha, Rais Kikwete pia
amezungumzia pia sheria ya makosa ya mitandao ambayo ameisaini hivi karibuni na
kusema kuwa uwepo wa sheria hiyo itakuwa ni mkombozi kwa wahanga wa matukio ya
uhalifu unaofanywa kupitia mitandao.
Rais Kikwete amewataka
watu wote ikiwa ni pamoja na mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia
kutoikosoa sheria hiyo, bali kupeleka mapendekezo yao mahali husika ili
yafanyiwe kazi kwa ajili ya maboresho ya sheria hiyo