‘Nikifa usije
kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi
za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki au majirani wakaapishana kwa maneno hayo,
walitafutwa wazee wenye hekima ili kuondoa laana hiyo.
Sasa, hivi karibuni, baada
ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio
katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno
hayo yametumika pasipo sababu,
AUNT BILA
KUUMA MANENO
Juzi, Aunt
ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga
dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na
kuomboleza.
KIASA CHA
KAULI
Kauli hiyo ya
Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo
akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata
akifa, Aunt asiende kumzika.
MSIKIE
AUNT ‘LAIVU’
Ijumaa
wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa
kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende
kumzika. Wewe unasemaje?
Aunt: Kwanza
nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake
nimesikia wanaongea mambo kibao.
“Ila mimi
sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji
yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata
mimi nasema sitamzika Wema.
AANZA
KUFUNGUKA
”Halafu
sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo
nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.
ILIKUWA
UTANI, IYOBO ATAJWA
“Mimi sidhani
kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani
lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa
kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la
muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa
asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na
familia yangu niishi,” alisema Aunt.
FAMILIA
YAWEKA KIKAO
Kufuatia
vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni familia ya Wema inadaiwa kuweka
kikao na kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia
kuwa, urafiki wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini
hautadumu kwa sababu ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.
Chanzo makini
kutoka katika familia ya Wema kimelipenyezea ubuyuIjumaa Wikienda ambapo
kilitiririka:
“Mama Wema
kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema kwa sasa hataki tena kumwona
mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu ni mnafiki.
MAAZIMIO YA
KIKAO YAFIKA KWA WEMA
“Maneno hayo
ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa Wema, akawaelewa na kusema hana haja
tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee nini maana hakuna anachomsaidia.”
Aunt
alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema na jinsi staa huyo
alivyoyapokea, alisema:
“Kama
familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana
nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya
wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu
tena wanajitambua kwa kila hali.
“Nikiangalia
sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana
haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi
nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.
“Kama staili
ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana
mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa
kuburuzwa hivyo.
“Kama
wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya
kujipendekeza kwao.
WEMA
AZIDI KUCHAMBULIWA
“Hakuna kitu
kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu
basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na
wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye
akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”
WEMA
NAYE ATEMA NENO
Baada ya Ijumaa
Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na
kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:
“Yaani hata
sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye
ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia
yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.
“Sifikirii
kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana
alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”
Aunt
‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana
baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari
All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe
shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo
lililomkera Wema akiamini Aunt ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu
wake hao.