Wednesday 29 April 2015

Watu 69 wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuchoma kanisa nchini Misri


Mahakama ya Misri imewahukumia kifungo ncha maisha jela, watu 69 baada ya kupatikana na hatia kuchoma kanisa moja nchini humo.

Kanisa hilo liliteketezwa moto wakati machafuko yalipozuka eneo la Kerdasa karibu na mji wa Cairo mwaka 2013.

Makabiliano makali yalizuka pale jeshi lilipoanza kuwaondoa wafuasi wa aliyekua Rais Mohammed Morsi kutoka maeneo waliokua wakiandamana.


Mamia ya waandamanaji waliuawa kwenye operesheni hiyo.