Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari
yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita
ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.
Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.