Wednesday, 15 April 2015

Mke wa Mwanamuziki SHETTA Adai Talaka, Kisa Rose Ndauka


Siku chache baada ya habari ya staa wa Bongo Fleva , Nurdin Bilal ‘Shetta’ kudaiwa kulala chumba kimoja na staa wa Bongo Movies, Rose Ndauka kuandikwa gazetini, mkewe Neila Yusuf ameshindwa kuvumilia na kudai talaka yake, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Shetta na Rose waliripotiwa na “gazeti pendwa”moja kuwa walilala katika chumba kimoja katika Hoteli ya Kingway iliyopo mkoani Morogoro walipokuwa wamekwenda kwenye mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya gazeti hilo kusambaa mtaani na mke wa Shetta kufikishiwa nakala yake na wapenda ‘ubuyu’, kilinuka ile mbaya nyumbani kwa Mbongo Fleva huyo, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke aliamua kudai talaka yake.

Mke huyo wa Shetta ambaye wamebahatika kupata mtoto mmoja na msanii huyo (Kayla) alimjia juu mumewe na kutaka amwambie ukweli wa habari hiyo jambo lililoleta tafrani hadi kufikia hatua ya kutimka nyumbani hadi wazazi wa pande zote mbili wakalazimika kuweka vikao vya usuluhishi.

Licha ya jitihada hizo kutoka kwa wazazi, bado mama Kayla alikataa kusuluhishwa na kudai hasira zake zitashuka mara atakapokutana na Rose uso kwa uso.“Kilinuka kiasi cha mke wa Shetta kufungasha virago huku akisisitiza kwamba kabla ya kuondoka mazima atahakikisha anamfungia kazi Rose ili aweze kumweleza kinaga ubaga juu ya ilikuwaje akapindua na mumewe chumba kimoja,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa  Rose na kuulizwa kama amepata taarifa za kutafutwa na mke wa Shetta na kuhusu kuhusishwa na tukio hilo ambapo alijibu kuwa hajapata taarifa.“Mimi sijapata hizo taarifa, kama ananitafuta mimi nipo tu maana sijafanya kosa lolote. Kama nilivyosema awali, kweli nilisafiri na Shetta kwenda Morogoro na tulilala hoteli moja lakini vyumba tofauti, Shetta namheshimu siwezi kufanya naye jambo kama hilo,” alisema Rose.

 Shetta  kwa upande wake  alipotafutwa ili kujua ukweli wa tukio hilo ambapo alikiri kumtokea na kuwashushia lawama wambeya.“Ni kweli mke wangu amekerwa sana na habari zile, kuna wambeya ndiyo wamemjaza maneno kiasi cha kuleta tafrani hadi wazazi kuingilia kati ingawa mimi naamini haya ni mambo ya kifamilia tu ambayo mke wangu atayaelewa na yataisha tu.

Mke wangu ni muelewa sana, nampenda na ananipenda, hii hali ni ya kawaida kwa wanandoa ila kwa kuwa mimi ni msanii mke wangu atajua tu kuwa watu wanaongea sana juu yetu,” alisema Shetta.

GPL