Tume ya Uchaguzi wa taifa la Tanzania, kukabiliwa na
na msisitizo wa muda mrefu wa wananchi juu ya kuahirishwa kwa tarehe ya
kufanyika kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekzwa na tume hiyo kutoa msimamo
kwamba tarehe haitobadilika, leo hii tume hiyo imetoa kauli tofauti. Mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametangaza kuwa zoezi hilo la
kura ya maoni limeahirishwa, jambo ambalo limezua hisia tofauti nchini humo.