Sunday, 12 April 2015

DIAMOND : "I'd Rather Die Than Go Back To Wema Sepetu"


Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.

Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kukutana na Diamond uso kwa uso ambaye alithibitisha taarifa ambazo zilielezwa na mtu wake wa karibu:

“Umeambiwa na nani hayo? Sipendi kuongelea sana hivi vitu lakini huo uliousikia ndiyo ukweli. Kwa sasa nawaza maisha yangu na mpenzi wangu Zari baada ya kupitia majaribu mengi kimapenzi enzi hizo.

“Huenda wengi wasiamini ninayosema lakini nafsi yangu haijawahi kuniongoza kukumbuka ya nyuma tena kama ilivyowahi kutokea awali.

“Wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili lakini sikupenda kujibu kwa kuwa nilihisi litaleta tafrani kwa mashabiki wangu, sioni sababu ya kuendelea kuulizwa kwenye media hivyo ukweli ni kwamba siwezi kurudi nyuma tena,” alisema Diamond

Source: gazeti la Risasi