Staa mwenye ‘figa’
matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake
aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii
wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.
Ishu
ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima
ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii
huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu
mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.
“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote
tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua
ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema
Amanda.