Wednesday, 11 March 2015

MTIFUANO BARAZA LA WAWAKILISHI KUHUSU KURA YA MAONI - KATIBA PENDEKEZWA



Leo kulikuwa na sinema pale BLW.Kwanza mswaada wa kura ya maoni umewasilishwa na waziri ofisi ya rais muungano bada la ya waziri wa sheria mwenye dhamana ya katiba na sheria. Pili kulikuwa na mabishano ya hoja kati ya mwanasheria mkuu, Mh jussa na spika.

Mwanasheria mkuu.
Hoja ya kura ya maoni ni mwendelezo tu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo ilisharidhiwa na si jambo jipya hivyo kashauri haijadiliwi inahitaji kuridhiwa kwa sababu inazungumzia jambo la muungano ambalo kwa maelezo yake Baraza halina mamlaka ya kuzuiya.


Mh Spika
ilikuwa lazima iletwe iridhiwe ili kwenda sambamba na utaratibu wa sheria za Zanzibar. hata hivyo kasema suala hili ni muendelezo. alikuwa anakwenda mbele mara anarudi nyuma.


Mh Jussa.
Alisema katiba ya Zanzibar imeshaitangulia Sheria hiyo kwa sababu imeshaweka masharti ya kura ya maoni Zanzibar. Amesema baraza limeshawahi kukataa mambo ya aina hio kwa mambo yasiyo na maslahi na Zanzibar.


Amesema sheria ya kura ya maoni na sheria ya mabadiliko ya katiba ni vitu viwili tofauti.Inahitaji kujadiliwa na kwa Zanzibar katiba yake imeshaweka masharti kauliza kwa nini suali hili linataka kulazimishwa wakati huko nyuma baraza liliwahi kukataa mambo ya aina hii?
amotoa mifano ya sheria ya haki za binadamu na bahari kuu ilikataliwa na Zanzibar ikaja na sheria zake.


Si Spika wala Mwanasheria mkuu aliyeweza KUJIBU KITU. WAMELAZIMISHA TU. amesema hatakama bahari kuu ni jambo la muungano lakini halikujumuishwa tu kwamba HALIWEZI KUJADILIWA NA BARAZA LA WAWAKILISHI KWA SABABU NI JAMBO LA MUUNGANO mbona LILIJADILIWA NA KUKATALIWA NA BLW IWEJE HII YA KURA YA MAONI? KIMYA.

Hapo ikawa Spika anataka kulazimisha ikiwa inaungwa mkono au la ndipo CUf wakasimama na kupiga meza. Mchezo uliendelea eti Mwanasheria mkuu atoe hoja ndani ya makelele na sintofahamu mara ikasemwa hoja imeungwa mkono. wakati huo kelele zikiendelea, mawaziri na manaibu waziri wanaotokana na CUF wakiwa wametoka kuashiria kutounga mkono filamu hiyo na wakati huo huo Waziri wa sheria Bwana Abubakari akiwa kasimama kuomba kutoa maelezo bila ya kupewa nafasi na SPIKa mwisha akaamuwa kutoka.