Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.
Akizunguma na waandishi
wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la
kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati
hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au
kundi fulani.
Amesema watu wengine
wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa
na suala la mauji ya watu wenye ualbino.
Matembezi hayo
yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe
wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu
hao wenye Ualbino.
Akizungumzia Matembezi
hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo
hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.
mdimu amesema kuwa
harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino
ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.
"Hatulengi masuala
ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo
washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika
familia"amesma Mdimu.
Amesema harakati hizo
zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza
kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia
kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni
Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania
Bloggers Network,Joachim Mushi.
Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya
habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani
yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam
na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine
pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim
Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki
Mkongwe nchini,Jhiko Manyika "Jhikoman".
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha
waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya
Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.