Wednesday, 15 April 2015

NI MAJONZI KATIKA SOKA TENA: MCHA KHAMIS AFARIKI DUNIA


Kiungo wa Azam FC na Taifa Stars Khamis Mcha ‘Vialli’ (pichani) amefiwa na baba yake mzazi, Mcha Khamis, mchezaji wa zamani wa KMKM.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Zanzibar, Mcha Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Baba huyo wa kiungo wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Khamis Mcha ‘Vialli’
 amefariki duniani mjini Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake, Mcha mkubwa alichezea klabu za 
KMKM na Miembenipamoja na timu ya taifa ya Zanzibar. Pumzika kwa amani Mcha Khamis, ahadi yako imetimia.