BW. LEODGAR TENGA NA RAISI WA SASA WA TFF JAMAL
MALINZI
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.
NB: Kesho alhamisi saa 5 kamili asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TFF uliopo Karume, makocha wa Twiga Stars na She-Polopolo wataongelea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa siku ya ijumaa.