Friday, 17 April 2015

Diamond: Zari kaniweka kwenye kiganja

Msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul (Diamond Platnumz), amesema ujauzito aliobeba Zarina ‘Zari’ anaona kama amewekwa kwenye kiganja cha mchumba wake huyo.
Diamond alisema licha ya kutokuwa na fikra ya kuwa na maisha ya kujenga familia na msichana huyo wa Uganda, ila ujauzito alionao unaotarajiwa kumletea motto umekuwa chachu kubwa ya kuongeza mapnezi kwa Zari.
“Sikutegemea kuwa na Zari, lakini kwa hali aliyonayo sasa ya ujauzito ni kama ameniweka kiganjani  na sasa ninachoomba motto azaliwe salama na awe na akili nyingi” Alisema Diamond.
Diamond aliongeza kwamba wasichana wengi aliowahi kuwa na uhusioano nao walikosa vitu vya kufanana naye.
“Niliokuwa nao nadhani kulikuwa na vitu ambavyo havikukamilika, ndiyo maana hatukuwa tukiishi kwa muda mrefu na kuanzisha maisha kama haya na Zari,” alisema diamond.