Basi la Luwinzo na basi ndogo la Masanga Line Express
zimepata ajali kwa kugonga katika hifadhi ya Mikumi barabara kuu ya
Iringa-Morogoro na kusababisha watu saba kupoteza maisha papo hapo huku wengine
17 wakijeruhiwa katika tukio lililotokea leo majira ya saa 6 mchana mkoani
Morogoro.
Ajali hiyo ni ya pili ndani ya siku
mbili baada ya ajali nyingine katika hifadhi hiyo ikihusisha basi la FM
Safari na Fuso kutokea marchi 17 majira ya saa 5:30 asubuhi na
kusababisha watu wawili kufariki dunia na wengine nane kujeruhiwa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Morogoro Leonard Paulo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na
utelezi ukichangiwa na mwendo kasi hali iliyomfanya dereva wa basi ndogo
la Msanga Line Express kushindwa kulimudu vyema gari na kwenda
kuligonga basi la Luwinzo lililokuwa likitokea Njombe kuelekea Dar es
Salaam.