Friday 10 April 2015

REVEALED: CHADEMA Yapanga Kupenyeza Mamluki ACT - Wazalendo!


Baada ya Zitto kutoa kauli kwa vyombo vya habari kuwa, kuna zaidi ya wabunge 50 kutoka vyama vya CCM na CHADEMA watakao hamia ACT, CHADEMA kupitia kitengo chake cha intelijensia kimetangaza upelelezi rasmi ili kuweza kuwavumbua wabunge hao wasaliti wa chama na mamluki wengine!

Aidha, maofisa hao katika kitengo hicho cha intelijensia cha CHADEMA wameeleza wazi kuwa wanaifanya kazi hiyo kwa usahihi na umakini mkubwa ili kuhakikisha taarifa watakazokusanya ni za kweli huku wakielezea mkakati wao wa kupenyeza watu wao ndani ya ACT kwa ajili ya taarifa zaidi!

My take,

Kwa hali hii, nadhani CHADEMA imeanza kusahau jukumu lake la msingi la kufanya siasa na kujenga chama, badala yake nguvu nyingi zaidi imeelekezwa kwenye kusaka hao wanaoitwa 'wasaliti'!

Mbona CCM ina watu wanatofautiana kimtazamo lakini maisha ya siasa yanaenda kama kawaida na hatusikii majina majina kama wasaliti?