Thursday, 19 March 2015

TID JELA YAMUITA BAADA YA KUHUSISHWA NA MSALA MWINGINE



ISSA MNALLY/Amani11
HAJAKOMA? Staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Chumvini, Khaleed Mohamed ‘TID’ amehusishwa na msala mwingine baada ya kudaiwa ku kumjeruhi James Richard, mkazi wa Jiji la Dar.


.
Khaleed Mohamed ‘TID’.
Alisema wakati anashambuliwa na TID, Dulla aliwaambia watu waliokuwepo kuwa wasiamulie na ambaye angekaidi  angemchoma kisu cha chembe ambapo waliogopa mpaka alipofika mjumbe wa mtaani huo, akaamulia.

Alisema kuwa TID alimpiga kiasi ambacho uso ulivimba, kuteguliwa mkono na kuchomwa visu kichwani na kisogoni ambako alitokwa damu nyingi hadi  wasamaria wema walipoungana na mjumbe kumsaidia kisha kumkimbiza Kituo cha Polisi cha Oysterbay damu zikiwa zinamtoka chapachapa ambako alipata hati ya polisi ya matibabu (PF3) na kufungua kesi iliyosomeka OB/RB/3211/2013.

Kitendo hicho kiliwakasirisha polisi waliokuwa zamu ambapo mmoja wao alisema anamshangaa TID kurudia kosa lililompeleka gerezani huko nyuma.James alisema baada ya kufungua kesi hiyo, alikimbizwa katika Hospitali ya CCBRT ambako alishonwa nyuzi nne katika jeraha la kisogoni na kupatiwa dawa kwa ajili ya maumivu ya mkono na usoni ambako alivimba sana.

“Leo naenda (Jumanne) naenda tena hospitali ili nijaziwe PF3 yangu kwa ajili ya kulipeleka shauri hili mahakamani,” alisema James kwa masikitiko.Jitihada za kumpata TID anayesakwa na jeshi la polisi ili kusikia kauli yake kuhusiana na madai hayo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.
Hata hivyo, waandishi wetu wanaendelea kumtafuta.

Chanzo: GPL